TANZANIA NA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 28, 2016.

Habari, michezo na udagu ndio habari ambazo zimetawala vichwa mbalimbali katika magazeti ya leo, pitia kujipatia habari zilizojiri.



























MALI ZA CUF ZAKAMATWA.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi za chama hicho cha siasa hapa nchini kwenye ofisi yao Buguruni jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa habari na uenizi wa CUF taifa Bw. Abdul Kambaya amesena magari hayo yamekutwa yakiwa yamefichwa kwa kada mmoja wa Chama kimoja maatufu hapa nchini kwa  sababu zisizoeleweka.

Kukamatwa kwa nagari hayo kunafuatia mpasuko uliotokana  na tofautina kiuongozi ndani ya chama hicho ambapo upande mmoja unamtii Katibu Mkuu wake Maalim Seif Sharif Hamad huku upande mwingine ukimtii Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba.

Tofauti hizo ndio zilizozaa wazo la kurejeshwa kwa Mali zote za chama hasa baada ya kubaini kuwa sehemu ya mali hizo zipo mikononi mwa viongozi waandamizi.

NYEGERE NI MNYAMA HATARI.

Nyegere ni mnyama asiyeogopa chochote mile kwani anauwezo wa kuwakabili wanyama wakali na wakubwa kama simba au chui na wasimdhuru, ni mmoja kati ya wanyama wenye wivu sana duniani.

Nyegere anangozi wanangozi ngumu ambayo hata zana za jadi kama mishale au mkuki hazipiti pia ana meno makali na magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe.

Mnyama huyu hupenda sana asali na huwa mkali sana pale anapogungua umegusa mzinga wa asali aliouachia hatufu yake atakufuata popote pale ulipo hadi akupate na kulipiza kisasi.

Hupatikana zaidi katika maeneo ya Afrika Mashariki na kati.

WANAWAKE WAMEGOMA KUKAA NYUMBANI NA KULEA WATOTO.

Mkoani Mtwara wanawake wameamua kuchukua pikipiki na kuendesha kwa lengo la kufanya biashara ijulikanayo kwa jina maarufu kama bodaboda.

Wanawake hao wamekuwa wakiaminiwa zaidi na wananchi kwa kuwa wanaendesha vyombo hivyo vya moto kwa utaratibu na kwa umakini was hali ya juu.

BABA YAKE Mh. MIZENGO PINDA AFARIKI.

Baba mzazi wa waziri mkuu mstaafu Mh. Mizengo Linda, Mzee Xavery Kayanza Linda amefariki dunia Leo majira ya saa 9:30 alasiri katika hospitali ya mkoa wa Dodoma maarufu kwa jina la hospitali ya General akiwa na miaka 90.

"Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la  Bwana libarikiwe"

LIVERPOOL YAPATA PIGO.

Liverpool itapitia katika wakati mgumu kama mshambuliaji wao maarufu Phillipie Coutinho hatarudi mapema uwanjani, hii ni kutokana na majeraha aliyopata dhidi ya club ya Sunderland.

Haijafahamika mpaka sasa mchezaji huyo mwenye uraia wa nchini mbazili amepata majeraha yenye ukubwa gani na bado haidhibitishwa rasmi atakaa nje ya uwanja kwa kipindi gani japo kwa mtazamo wa haraka mchezaji huyo amepata majeraha makubwa.

NANI KUWA MCHEZA BORA WA BBC 2016?

November 28 mashabiki wote kutoka kila kona ya dunia watapiga kura kumchagua mchezaji bora wa mwaka wa BBC.

Wafuatao ndio wachezaji ambao wanawania tuzo hizo ambao wanachezi ligi mbalimbali barani ulaya huku wengi wao wakitoka katika ligi kuu ya nchini England na mchezaji mmoja tu ndio anayetoka katika ligi kuu ya nchi Ujerumani.

Nao in:-
Aubameyang.
Andre Ayew.
Riyad Mahrez.
Sadio Mane.
Yaya You're.

H. E SAMIA SULUHU HASSAN

 Baada ya kifo cha aliyekuewa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayari John Pombe Joseph Magufuli, aliekuwa makamu wake mama Samia S...