DAKIKA 10 ZAIPAISHA SERENGETI BOYS VS GHANA.

Dakika 10 za mwamuzi zaipaisha Serengeti boys kwa kupata sare ya magoli mawili kwa mawili dhidi ya wapinzani wao Ghana ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa vijana wa umri chini ya miaka 17.

Baada ya dakila ya 21 na 75  vijana hao was Ghana walijipatia magoli yao kupitia kwa Sulley Ibrahim na Arko Mensah na kufanya dakika zote 90 Ghana kuwa mbele kwa magoli 2.

Kutokana na wachezaji wa Ghana kuanguka mara kwa Mara na kusababisha dakika nyingi kupotea ndipo mwamuzi akaongeza kakika 10 na kuifanya Serengeti boys kuzitumia dakika hizo vizuri kwa kujipatia magoli mawili huku moja kati ya hilo likifungwa kwa njia ya tuta baada ya beki was Ghana kuunawa mpira katika harakati za kuokoa.

Magoli ya Serengeti boys yalifungwa na Assad Juma kwa njia ya tuta, huku furaha ya watanzania ikirudishwa na Muhsin Makame kwa kufunga goli la pili katika dakika za mwisho za mchezo na kufanya matokeo kusomeka 2-2 mpaka mwisho wa mchezo.

No comments:

Post a Comment

H. E SAMIA SULUHU HASSAN

 Baada ya kifo cha aliyekuewa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayari John Pombe Joseph Magufuli, aliekuwa makamu wake mama Samia S...