TAHLISO YATOA WIKI MOJA KWA SERIKALI KUTOA MIKOPO.

Shirikisho la serikali za wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) limetoa muda wa wiki moja kwa wanafunzi waliokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo vyote ikiwemo uhitaji kusikilizwa na serikali kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.

Tamko hilo limetolewa Leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwana Stanslaus Peter, katika kikao cha pamoja kilichohusisha marais was vyuo vyote nchini, waliokutana jijini Dar es salaam Leo, kujadili sintofahamu inayowakumba wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali nchini.

Stanslaus amesema kuwa kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanufaika, na wengine kunyimwa kabisa ama kwa visingizio au bila sababu, jambo linalowafanya waishi katika mazingira magumu na kuhatarisha hatma yao kimasomo.

Amesema wamekubaliana kuwa, endapo serikali haitafanya kazi ombi hilo ndani ya wiki moja, basi shirikishi hilo litachukua hatua ikiwa ni pamoja na  kuhamasisha wanafunzi was mwaka wa pili na watatu kuungana na wale wa mwaka was kwanza katika kudai haki yao.

No comments:

Post a Comment

H. E SAMIA SULUHU HASSAN

 Baada ya kifo cha aliyekuewa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayari John Pombe Joseph Magufuli, aliekuwa makamu wake mama Samia S...